Shule za msingi 38 zimefutiwa matokeo ya darasa la saba baada ya kufanya udanganyifu.

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limefuta matokeo ya mitihani ya Taifa ya darasa la 7 kwa shule 38, ambazo zimebainika kufanya udanganyifu kwenye mitihani hiyo iliyofanyika Oktoba 7 na 8, 2020, na kuwafutia matokeo watahiniwa 1,059, baada ya kubainika wamefanya udanganyifu. Taarifa hiyo imetolewa hii leo Novemba 21, 2020, na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo